The United Republic of Tanzania

TANZANIA INVESTMENT CENTRE“Uchumi wa uwekezaji kwenye mifuko mbadala ni mkubwa kuliko uchumi unaotokana na uwekezaji kwenye mifuko ya plastiki” – Mhe. J. Y Makamba (MB) .


‘Kwa mujibu wa Kanuni za Sheria ya Mazingira, Serikali imetoa tamko la katazo la mifuko ya plastiki nchini kunzia kwenye kuzalisha, kuuza ndani na nje ya nchi, kuingiza nchini kutoka nje ya nchi, kumiliki, kuhifadhi, na kutumia. Atakayekiuka Sheria hiyo, atapata adhabu.’

 

Ni ujumbe mzito uliotolewa kwa Wananchi kupitia kikao cha wadau  kilichofanyika tarehe 15 Aprili, 2019 kuhusu fursa za uwekezaji katika uzalishaji wa mifuko mbadala ya plastiki kwenye ukumbi wa Kimataifa wa Julius Nyerere, Dar es Salaam. Lengo la kikao lilikuwa ni kuhamasisha Wadau kuhusu uzalishaji wa mifuko mbadala wa mifuko ya plastiki ili kuhifadhi mazingira. Kipekee kabisa kikao hicho   kilihudhuriwa na Waheshimiwa Mawaziri watatu ambao ni  Mhe. Angellah J. Kairuki, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Uwekezaji;  Mhe. Joseph Kakunda, Waziri wa Viwanda na Biashara  na Mhe. Januari Makamba, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais, Mazingira ambaye alikuwa mwenyeji wa mkutano huo.

 

Hotuba za viongozi zimefafanua kuwa, mifuko ya plastiki ni hatari kwa mazingira na afya za viumbe hai. Akitolea mfano Mhe. Makamba ameeleza kuwa takwimu za sasa zinaonesha kiasi cha tani 73,000  hadi 76,000 za mifuko ya plastiki huzalishwa nchini wakati tani 300,000 za plastiki kwa mwaka huingizwa nchini. Kutokana na madhara yanayoambatana na matumizi ya mifuko hiyo, Mhe. Makamba amebainisha kuwa jitihada za kuondoa mifuko  hiyo zilianza mwaka 2003 lakini hazikuzaa matunda na mdahara yake yaliendelea kuongezeka. Kufuatia hatua hiyo, Serikali ilitoa uamuzi wa kuzuia uzalishaji na usambazi wa mifuko ya plastiki mwezi Agosti, 2016. Hata hivyo wadau waliomba kupewa muda wa maandalizi hadi tarehe 30 Desemba, 2017. Kwa marejeo hayo  tangazo la zuio la kuzalisha na kusambaza mifuko ya plastiki kuanzia tarehe 01 julai, 2019 siyo la kushtukiza.

 

Kutokana na tafiti za kitaalamu zilizokwishafanyika zimeeleza kuwa kuendelea kuruhusu matumizi ya mifuko hii, vilevile ni kuendeleza uharibifu wa mazingira na kuleta athari kwa viumbe hai.  Serikali imemedhamiria kupiga marufuku nchini mifuko ya plastiki ya  kubebea vitu (Plastic Carrier Bags) huku vifungashiyo vya bidhaa kama korosho, maziwa, mazao ya kilimo, madawa, na bidhaa ya viwandani havijapigwa marufuku.

 

Kufuatia zuio hilo, changamoto kwa sasa ni kuongeza uzalishaji katika muda uliopo hadi ifikapo tarehe 01 Julai, 2019. Ili kufanikisha utekelezaji wa uamuzi huu, Wadau wa uzalishaji wa mifuko mbadala wanategemewa sana amezungumza Mhe. makamba.  Akitoa neon kwa Washiriki wka niaba ya Wadu wa Uwekezaji, Mhe. Kairuki ametoa wito kwa wawekezaji Wazawa na Wageni kutumia fursa hii kuwekeza katika uzalishaji wa vifungashiyo na mifuko mbadala ya plastiki. Vilevile amelitaka Shirika la Viwanda Vidogovidogo (SIDO) kuzalisha mashine za kutengeneza vifungashiyo na mifuko mbadala  huku  Kampuni ya SPM Mgololo na Wakala wa Misitu Tanzania imeelekezwa kuongeza kasi ya uzalishaji ili kuwawezesha wawekezaji kupata  malighafi za kutosha.

 

Kwa upande wake Mhe. Kakunda ameelezea kuwa uchumi unatafasiriwa kama ardhi na anga ambapo kwa ujumla wake ni mazingira. Ili uchumi uendelee unahitaji mazingira bora. Hivyo  kuwekeze  kwa  kuzingatia utunzaji wa mazingira endelevu kwa maendeleo ya uchumi wa leo na wa  kizazi kijacho.

 

Mwisho, Wadau wenye nia ya kuwekeza kwenye  miradi ya kuzalisha mifuko mbadala ya mifuko ya plastiki wanakaribishwa  kushirikiana na  taasisi muhimu ili kuepusha usumbufu usiokuwa wa lazima. Taasisi hizo ni   Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC), Mamlaka ya Viwango Tanzania (TBS); Baraza la Taifa la Usimamizi wa Mazingira (NEMC) , Shirika la Maendeleo ya Viwanda Vidogo (SIDO) na Taasisi za Kifedha.

Social Medias

Copyright ©2018 Tanzania Investment Centre.
All Rights Reserved.
Designed, Developed, and Maintained by Tanzania Investment Centre(TIC)