The United Republic of Tanzania

TANZANIA INVESTMENT CENTRE

Balozi wa Tanzania nchini Ujerumani Mhe. Dkt. Abdallah Possi amefika nchini na ujumbe wa wafanyabiashara wawekezaji

Kituo cha uwekezaji Tanzania (TIC) tarehe 15 Julai, 2019 kimepokea ujumbe wa wafanyabiashara na wawekezaji kutoka Jamhuri ya Czech ambao umeongozwa/umeambatana na balozi wa Tanzania nchini Ujerumani Mhe. Dkt. Abdallah Possi; ambaye pia anasimamia Jamhuri ya Czech. Ujumbe huo kutoka Czech chini ya mwakilishi  wa Wizara ya Viwanda na Biashara Bw.Michal Prokop umetembelea Tanzania kwa ziara ya siku tatu tarehe 15-17 Julai, 2019 ili kujionea fursa za biashara na uwekezaji kwenye sekta mbalimbali.

Ukiwa nchini, ujumbe huo utakutana na Wizara/Taasisi/Mamlaka zinazosimamia sekta /maeneo ambayo  wameonesha nia ya kuwekeza ili kujadili fursa zilizopo na namna ya kushirikiana katika kufanikisha biashara na uwekezaji baina ya nchi hizi mbili. Vilevile, ili kuleta ufanisi zaidi , ujumbe huo pia utashiriki mikutano mbalimbali ya sekta binafsi ambayo imeandaliwa ili kuwawezesha kukutana na makampuni ya ya....

2019-07-15 17:40:55Kongamano la kimataifa la korosho limeandaliwa na TIC kushawishi wawekezaji wazawa na wageni kuwekeza kwenye uongezaji thamani zao la korosho

July,2019: Mkuu wa mkoa wa Mtwara Mhe.Gelasius Byakanwa amewakaribisha wawekezaji zaidi ya mia tatu (300) kutoka mikoa mbalimbali nchini na nje ya nchi kushiriki kongamano la kimataifa la uwekezaji katika sekta ya korosho. Kongamano hilo limeandaliwa na Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC) mahsus ili kushawishi wawekezaji wazawa na wageni kuanzisha miradi ya uwekezaji nchini kwenye zao la korosho katika eneo la ubanguaji/ kuongeza thamani. Kongamano limefanyika kwa siku mbili tarehe 12 na 13 Julai, 2019 kwenye ukumbi wa BOT, Mtwara. Eneo la kuongeza thamani limepewa kipaumbele nchini ili kuwezesha uzalishaji wa bidhaa zinazotokana na korosho yenyewe, mabibo, maganda na kujengwa kwa viwanda vya kuzalisha pembejeo za korosho tukilenga kuleta tija zaidi kwa manufaa ya watanzania na Taifa kwa ujumla. Baadhi ya bidhaa zinazotokana na zao la korosho ni pamoja na....

2019-07-15 14:20:20Notice to all investors; Land rent arrears and facilitation fee on derivative titles issued by Tanzania Investment Centre (TIC)

                                                      TANZANIA INVESTMENT CENTRE

                                                                Notice to all investors

  Land rent arrears and facilitation fee on derivative titles issued by Tanzania Investment Centre (TIC)

The Executive Director of Tanzania Investment Centre (TIC) would like to kindly remind all Investors with Derivative Titles of their obligation to pay outstanding land rent arrears owed to the Ministry of Lands, Housing and Human Settlement Development and TIC facilitation fee for the financial year 2018/2019....

2019-07-05 11:47:39Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC) kinashiriki kwenye maonesho ya Sabasaba 2019 ili kutoa ufafanuzi wa kujisajili na Kituo na faida za huduma zake kwa mradi.

Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC) kinashiriki maonesho ya 43 ya Kimataifa ya Biashara ya Dar es Salaam (DITF) maarufu kama Sabasaba yanayofanyika kwenye viwanja vya Mwalimu Julius Nyerere Barabara ya Kilwa, Dar es Salaam kuanzia tarehe 28 Juni -tarehe 13 Julai, 2019. Kauli mbiu ya maonesho ni 'usindikaji wa mazao ya biashara kwa maendeleo endelevu ya biashara'. Kauli mbiu imelenga kuunga mkono jitihada za Serikali ya Awamu ya Tano chini ya Rais Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli inayohimiza uanzishaji wa viwanda vya usindikaji nchini.

Katika kutekeleza kauli mbiu ya maonesho ya Sabasaba 2019, Kituo kinawahamisisha wawekezaji wazawa na wageni kuanzisha miradi ya uwekezaji inayolenga kuongeza thamani mazao ya kilimo ili kuzalisha bidhaa kama vile juice, mvinyo, mafuta ya kula, unga, dawa, maziwa, chakula cha mifugo, samaki na uzalishaji wa....

2019-07-03 13:55:40Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC) kinashiriki kwenye maonesho ya Sabasaba 2019 ili kutoa ufafanuzi wa kujisajili na Kituo ili kunufaika na huduma zake.

Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC) kinashiriki maonesho ya 43 ya Kimataifa ya Biashara ya Dar es Salaam (DITF) maarufu kama Sabasaba yanayofanyika kwenye viwanja vya Mwalimu Julius Nyerere Barabara ya Kilwa, Dar es Salaam kuanzia tarehe 28 Juni -tarehe 13 Julai, 2019. Kauli mbiu ya maonesho ni 'usindikaji wa mazao ya biashara kwa maendeleo endelevu ya biashara'. Kauli mbiu imelenga kuunga mkono jitihada za Serikali ya Awamu ya Tano chini ya Rais Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli inayohimiza uanzishaji wa viwanda vya usindikaji nchini.

Katika kutekeleza kauli mbiu ya maonesho ya Sabasaba 2019, Kituo kinawahamisisha wawekezaji wazawa na wageni kuanzisha miradi ya uwekezaji inayolenga kuongeza thamani mazao ya kilimo ili kuzalisha bidhaa kama vile juice, mvinyo, mafuta ya kula, unga, dawa, maziwa, chakula cha mifugo, samaki na uzalishaji wa....

2019-07-03 13:53:51
Social Medias

Copyright ©2018 Tanzania Investment Centre.
All Rights Reserved.
Designed, Developed, and Maintained by Tanzania Investment Centre(TIC)