The United Republic of Tanzania

TANZANIA INVESTMENT CENTRETIC YAKUTANISHA WADAU WA TAASISI ZA SERIKALI KATIKA KUJADILI CHANGAMOTO ZAUTOAJI WA HUDUMA KWA WAWEKEZAJI. .


Kituo cha Uwekezaji Tanzania TIC kwa mara ya nne mfululizo kimeweza kuitisha mkutano na wadau wa Taasisi za serikali zinazotoa vibali, leseni na huduma mbalimbali kwa wawekezaji ili kujadili kwa pamoja changamoto mbalimbali ambazo wawekezaji kwenye taasisi zao wanakutana nazo wakiwa wanahudumia wawekezaji.

The Council which will be chaired by the Executive Director Mr. Geoffrey Mwambe was launched on Friday at the Julius Nyerere Convention Centre by the Hon. Minister Mwijage.

Mkutano huo ambao huitishwa chini ya mwenyekiti ambaye ni Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Uwekezaji Bwana Geoffrey Mwambe umekuwa ni nguzo muhimu katika kutatua changamoto za wawekezaji. Akiongea na waandishi wa habari katika Mkutano huo, Mkurugenzi Mtendaji wa TIC ndugu Mwambe alisema kuwa kuna maboresho mengi ambayo yameweza kupatikana kutokana na uundwaji wa kamati hiyo ya Kitaifa ya kuhudumia wawekezaji na mpaka sasa zaidi ya changamoto 50 zimeweza kutatuliwa kwa kushirikisha wadau hao wa Taasisi za serikali chini ya Kamati hiyo ya NIFC.

Lendo ni kuhakikisha kuwa tunakabiliana na changamoto zote za wawekezaji na kuzitafutia ufumbuzi wa pamoja kwa haraka ili wawekezaji waweze kuwekeza miradi yao waliokusudia katika kipindi husika bila kukwamishwa na huduma na Taasisi zetu, alimalizia Mkurugenzi Mtendaji huyo.

Katika mkutano huo changamoto mbalimbali zimeweza kujadiliwa ikiwamo muda wa utolewaji wa vibali na leseni ili kuondoa ucheleweshwaji na kuboresha huduma, tozo mbalmbali, chngamoto za upatikanaji wa maeneo kwa ajili ya uwekezaji, huduma mbalimbali za vibali na leseni na mengi ambayo yanahitaji ufumbuzi wa taasisi hizo. Mkutano huo wa NIFC unafanyika kila mwezi na unahusisha viongozi wakuu wa Taasisi mbalimbali za serikali zinatoa huduma kwa wawekezaji wakiwamo Makamishna wa Kazi na Uhamiaji, TFDA, TBS, FCC, TANESCO, NEMC, AQRB, BRELA na taasisi nyingine nyingi zinazotoa huduma kwa wawekezaji.


Social Medias